Pages

Tuesday, April 8, 2014

MH:MWIGULU NCHEMBA APELEKEA UMEME VIJIJI 43 JIMBONI KWAKE

Mkuu wa Mkoa wa Singida(Kushoto) akibadilishana Mawazo na Waziri wa Nishati na Madini Mh:Sospeter Mhongo na Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba(kulia) hii leo baada ya Kuwasili Singida kikazi,Kubwa kutembelea Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini ndani ya Wilaya ya Iramba Jimbo la Mh:Mwigulu Nchemba.
 Waziri wa Nishati na Madini Mh:Mhongo akiwa na Mbunge wa Iramba Magharibi Mh:Mwigulu Nchemba mara baada ya Kufika Iramba Kijiji Cha Kaselya kwaajili ya Kuzungumza na Wananchi wa Kaselya kuhusu Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Kijijini Kwao Unavyoendelea na Wanavyopaswa Kujiandaa na Matumizi ya Umeme huo.
 Waziri wa Nishati na Madini akiwa na Mwenyeji wake Mh:Mwigulu Nchemba wakisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kaselya.Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda(kulia) akibadilishana Mawazo na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano na Wananchi wa Kaselya kuwaelezea Fursa waliyonayo kwenye Umeme walioingiziwa Kijijini Kwao.Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia na Wananchi Wake wa Kijiji cha Kaselya mara baada ya Kupokea Umeme na Kuwaelimisha Wananchi faida za Umeme huo.
Mh:Mhongo Waziri wa Nishati na Madini na Mh:Mwigulu Nchemba(Mb) wakishikana Mikono na Wakandarasi waliokabidhiwa Mradi huo wa Kusambaza Umeme Vijiji 43 ndani ya Jimbo la Iramba na Kukamilisha Mwezi wa Sita 2015 kwa Mkoa wote wa Singida.
 Mh:Mhongo akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kaselya hii leo Jimboni Iramba kuwaelimisha Mradi wa Umeme unaeondelea Kutekelezwa Kijijini Kwao.
Wananchi wa Kijiji Cha Mgongo Wakimlaki Mbunge wao baada ya Kuwaletea Umeme.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wake wa Kijiji cha Mgongo walionufaika na Umeme unaoendelea Kusambazwa Jimbo la Iramba takribani Vijiji 43.
"Mkataba wangu na Nyie ni Maendeleo tu,Haina Maana kuniona Mara kwa Mara Jimboni hapa bila Kuleta Maendeleo,Furahieni kuona Kazi Inatendekea na Maendeleo yanaonekana"Mwigulu Nchemba.Furaha ya Kutimiza Mahitaji ya Wananchi Wako,Mwigulu Nchemba akishangiliwa na Wananchi mara baada ya Kuwapa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Umeme na Miradi Mingine ya Maendeleo Kijiji Cha Mgongo.
 Sehemu tu ya Nguzo Nyingi Zilizosambwa kwenye Vijiji 43 Jimboni Iramba,Hizi zipo Kijiji Cha Mbelekesye.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliofika Kwenye Mkutano Kijiji Cha Mgongo kwaajili ya Kupatiwa Elimu ya Kupata Umeme na Kuutumia.Mh:Mhongo akimtambulisha Mkandarasi kwa Wananchi na Kuwaomba Kutoa Ushirikiano wakati wote wa Utekelezaji wa Mradi wa Umeme.
Wanafunzi wakiwa ni Wanufaikaji Wakubwa wa Umeme wakisikiliza Kwa Makini namna ya Kutumia Umeme huo.
 Mkoa Wa Singida husuasani Wilaya ya Iramba ni Watengenezaji wakubwa wa Mafuta ya Alizeti,Hapa Wanananchi wakitoa Zawadi zao za Mafuta kwa Mh:Mhongo na Mh:Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Nishati na Madini Mh:Sospeter Mhongo hii leo akiwa na Mwenyeji wake Mbunge wa Iramba Magharibi Mh:Mwigulu Nchemba Wametembelea Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Mkoani Singida kwa Wilaya ya Iramba.
Wilaya ya Iramba (JImbo la Mh:Mwigulu Nchemba) Mradi wa Umeme Vijijini Umevifikia Vijiji 43 katika Jimbo lote la Iramba,Mh:Mhongo amesema,Serikali imetenga Bilioni 31.9 kwa Mkoa wa Singida kuhakikisha Umeme unasambazwa sehemu Kubwa ya Vijiji ilikufungua Milango ya Kukua Uchumi na hatimaye Kuondokana na Umaskini.
Kwa Wananchi Watanufaika Zaidi na Mradi huo kwasababu Uunganishaji wa Umeme kwenye Makazi ni kwa Bei Nafuu sana,Mwananchi atatakiwa Kuchangia Tsh;27000(Elfu Ishirini na Saba tu) Kuunganishiwa Umeme Nyumbani Kwake tofauti na Kipindi cha Nyuma Umeme ulikuwa Unaunganishwa kwa Shilingi Laki nne na baadae Laki moja na Sabini.Hiyo 27000/= itakubalika tu endapo Mwananchi ataunganisha Umeme wakati Mkandarasi bado anaendelea na Ukamilishaji wa Mradi.
Akizungumza na Wananchi wa Mgongo,Mh:Mhongo amesema"Serikali ya CCM imedhamiria kufikisha Umeme kila Kona ya Nchi hii,Gesi tunayo ya Kutufanya tufikishe Umeme popote pale,Wananchi manaombwa Kuonesha Umoja wenu katika hatua hii ya MATOKEO MAKUBWA SASA ili Uchumi wa Nchi yetu ufikie pale tunapotakiwa Kufika.
Vilevile Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa Wananchi Wake kuchangamkia Fursa hiyo ya Kuunganishiwa Umeme kwa bei nafuu,Umeme wa bei nafuu Ulikuwa ni Historia kwa Nchi hii lakini sasa Umepatikana.Hivyo amewaomba Wananchi wa Vijiji Vyote 43 vinavyopitiwa na Mradi wa Umeme huo kujipanga Kutumia Umeme kwaajili ya Kuinua Uchumi wao.
"Mimi kazi Mkataba wangu na Nyie Wananchi nia Kuwaletea Maendeleo tu,Hivyo nitaendelea kuwaletea Maendeleo kadri ya Uwezo Wangu,Tuungane Mkono tufute Umaskini Kwa Wananchi wa Iramba" Mwigulu.
Baadhi ya Vijiji Vilivyopata Kunufaika na Mradi huo ni Mbelekesye,Mgongo,Kiselya,Mtoa,Kibaya na vingine vingi hatuwezi kuvitaja vyote

1 comment:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete