Pages

Saturday, April 12, 2014

Mh.Mwigulu Nchemba Akabidhi AMBULANCE kwa wananchi wa Tarafa ya Shelui

 
Hii ndio Gari ya Wagonjwa(Ambulance) aliyonunuliwa na Mh:Mwigulu Nchemba na Kuwakabidhi Wananchi wa Tarafa ya Shelui kwenye Kituo Kikubwa cha Afya cha Mgongo.Naibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe akijianda Kupanda kwenye Gari la Wagonjwa tayari kwa Kulizindua rasmi kwakaunza kutumika na Wananchi wa Tarafa ya shelui,Gari limenunuliwa na Mh Mwigulu Nchemba kwaajili ya Kituo cha Afya cha Mgongo.Naibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe Stephen Kebwe akionesha Ufungo wa Gari ya Wagonjwa na Kuukabidhi kwa Wananchi kupitia Mkurugenzi wao wa Wilaya.Mh:Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba akikabidhi kadi halali ya Umiliki wa Gari ya Wagonjwa kwenda kwa Wananchi.Naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi Ufunguo wa Gari Mkurugenzi wa Wilaya ya Iramba tayari kwa kuanza Kusimamia Matumizi ya Gari hilo mali ya Wananchi.Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Wananchi wa Kyengege waliojitokeza Kumpokea,Ameambatana pia na Mkuu wa Wilaya ya Iramba na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu NchembaNaibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe Stephen Kebwe akizindua rasmi Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba,Pia Kutoka Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda na Mbunge wa Jimbo hilo Mh:Mwigulu NChemba.Hii ndio Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Kyengege iliyozinduliwa na Naibu Waziri wa Afya.Kituo Cha Afya cha KyengegeNaibu Waziri wa Afya(Katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda na Mbunge wa Jimbo hilo Mh:Mwigulu Nchemba wakielekea kukagua maendeleo ya Kituo cha Afya cha Kyengege hususani kwenye kitengo cha Dawa.Wananchi wa Kata ya Kyengege wakifurahia Kupata Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya,Awali Wananchi hawa walipangisha Nyumba kwaajili ya Kuishi Watumishi hao.Mh:Lusinde Mbunge wa Mtera akizungumza na Wananchi wa kata ya Kyengege kuhusiana na Umuhimu wao Kushiriki kwenye kazi za Maendeleo hususani mambo ya Afya,Pia Kuwashuhudia namna Mh:Mwigulu Nchemba anavyolitumikia Taifa lake, Chama chake na hadi Jimboni Kwake.Amewasihi kutothubutu kuacha Kumuunga Mkono Mwigulu Nchemba,Wananchi Waendelee kumuunga mkono kipindi chote cha Uongozi wake."Msipende sana Kuiniona Mimi Mbunge wenu,Pendeni sana Kuona Maendeleo yanakuja na yanaonekana"Mmoja ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Kyengege(Jina hakufahamika) akifurahia Kupata Nyumba nzuri ya Kuishi.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Shelui kuhusu namna alivyotekeleza ahadi yake ya Kuwapatia Ambulance itakayosaidia Kuwahisha Wagonjwa kupata Matibabu kwenye Hospitali Kubwa za Igunga au Kiomboi-Iramba.
 Wananchi wa Kijiji cha Mgongo wakishangilia kwa Furaha mara baada ya Kukabidhiwa Gari ya Wagonjwa kutoka kwa Mbunge wao Mh:Mwigulu Nchemba.Katika Kata hii ya Mgongo,Mh:Mwigulu Nchemba wakati anaomba ridhaa ya Kuwaongoza Wananchi hawa aliwaahidi kuwapelekea Umeme,maji na Gari ya Wagonjwa,hadi sasa Mbunge huto ametekeleza Vyote alivyoahidi na amewaahidi kuanza kuwashughulikia uboreshaji wa Barabara.
Mamia ya Wananchi wa Shelui wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tendo la Kukabidhiwa Gari waliyopewa na Mbunge wao Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba.Naibu Waziri wa Afya Mh:Kebwe akimuchunguza Mama mwenye tatizo la tezi Shingoni na Kumuagiza Daktari wa Wilaya ya Iramba kuhakikisha anapekelekwa Hospitali kwa Matibabu zaidi.
 Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Mwananchi wa Kijiji cha Mtoa mwenye tatizo la tezi Kuvimba,Hapa akitoa fedha kwaajili ya Nauli ya Mama huyo kwaajili ya Kufuata Matibabu sehemu atakayopelekwa na Daktari wa Wilaya aliyeagizwa na Naibu Waziri wa Afya ahakikishe mama huyo anapata Matibabu Stahiki.Wananchi wa Kata ya Mgongo wakimpokea kwa Shangwe Mbunge wao Mh:Mwigulu Nchemba.

Katika hali inayoonekana ni Wazi kuwa Mh:Mwigulu Nchemba amejikita Kutimiza ahadi zake alizotoa kwa Wananchi wa Jimbo la Iramba,Hii leo amekabidhi Gari mpya ya Wagonjwa kwenye Tarafa ya Shelui Kituo cha Afya cha Mgongo.Hii ilikuwa ni moja ya ahadi zake wakati anaomba ridhaa ya Kuwaongoza Wananchi wake,Ameshawapelekea Umeme,Maji na sasa alimewakabidhi Gari ya Kubebea Wagonjwa katika Kituo hicho cha Afya.
Ikiwa ni Wiki moja tu tangu Mbunge huyo afanye Ziara na Mh:Waziri wa Nishati na Madini Mh:Mhongo kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme katika Vijiji 43 ndani ya Jimbo la Iramba Unaotegemewa Kukamilika Mwezi wa Sita 2015,Na Baadae Mbunge huyo ndani ya Wiki hiyo hiyo Moja alifanya ziara na Waziri wa Maji Mh:Maghembe na Kufungua baadhi ya Miradi ya Jimboni hapo Ukiwamo ule Mradi Mkubwa wa Maji Uliokamilika wa Nang'uli
Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea Kusisitiza kuwa Mkataba wake na Wananchi wa Jimbo la Iramba ni Shughuli za Maendeleo,alipewa ridhaa ya Kuwaongoza iliawaletee Maendeleo  kwa Vitendo,Hilo amekuwa akilifanya Jimbo la Iramba kwenye Seketa zote hususani Elimu,Afya,Umeme,Maji na Barabara.Kwa sehemu Kubwa ametekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi ndani ya Jimbo lake na sasa anajipanga Kujikita kwenye Kuboresha Barabara ya Kutoka Ndago Kupita Mbelekesye Kuja Singida,Kuboresha barabara ya Kidalu kuelekea Meatu n.k.
Kwa Nyakati tofauti Wananchi kwenye Mikutano ya hadhara wamekuwa wakishindwa kujizuia kutoa shukrani zao za dhati kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyowasaidia kwa muda mfupi tu kwenye shughuli za Maendeleo na Kwenye Kutatua Matatizo ya Watu binafsi na Jumuia.

  Source: MWIGULU NCHEMBA BLOG

No comments:

Post a Comment