Mkuu
wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, Edward Ole Lenga, akizungumza
kwenye hafla ya utundikaji mizinga ya nyuki kimkoa zilizofanyika katika
kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama.Wa pili kulia walioketi ni Mkuu wa
mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na (wa kwanza kulia) ni Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Mkalama, James. Kushoto (aliyekaa) ni Katibu
tawala mkoa wa Singida Liana Hassan.
Na Nathaniel Limu, Singida
KAIMU
mkuu wa wilaya ya Singida, Edward Ole Lenga, amewataka wakazi wa wilaya
hiyo wahakikishe wanahifadhi na kutunza vizuri chakula cha kutosha
mwaka mzima,ili kujikinga na balaa la njaa linatishia msimu huu kutokana
na mvua chache mno kunyesha.
Lenga
ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama,ametoa wito huo muda mfupi kabla
hajamkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, kuhutubia mamia
ya wakazi wa tarafa ya Mgori jimbo la Singida kaskazini kwenye kilele
cha maadhimisho ya siku ya kitaifa ya utundikaji wa mizinga ya nyuki
ambapo kimkoa yalifayika katika kijiji cha Pohama.
Alisema
mvua za msimu huu zimenyesha kwa kipindi kifupi mno na kukatika
mapema,kitendo kinachosababisha karibu mimea yote ikiwemo ya mazao ya
chakula kukauka kabla haijakomaa.
“Siku
zote mkuu wetu wa mkoa Dk.Kone amekuwa akiwahimiza wakulima kulima
mazao yaliyopewa kipau mbele na mkoa ambayo baadhi ni uwele,mtama na
jamii ya Kunde. Mazao haya na mengine yaliyopewa kipaumbele kwa vile
yanastahimili hali ya hewa katika mkoa wetu ambao ni ya ukame
unaosababishwa na mvua haba. Endapo msimu huu kutakuwa na mkulima
aliyelima Mahindi na zao lo lole ambalo halipo kwenye vipaumbele vya
mkoa, itakuwa imekula kwake”,alifafanua.
Alisema
kwa kifupi,msimu huu sio mzuri kwa upande wa kilimo kutokana na mvua
kukatika mapema na hivyo ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha i
wananchi wafanye juhudi mapema ya kuhakikisha wanakuwa na chakula cha
kukidhi mahitaji.
Aidha,Lenga
ametumia fursa hiyo pia kuwahimiza wafugaji wa mifugo kuuza baadhi
mapema,ili waweze kununua chakula/nafaka kitakachokidhi mahitaji ya
mwaka mzima.
Akifafanua
zaidi,alisema “ukame wa mwaka huu, umesababisha pia kuwepo kwa uhaba
mkubwa wa malisho ya mifugo na maji pia. Hali hii inaweza kusababisha
mifugo kukonda na hivyo baadae itakosakabisa soko zuri au isiuzike
kabisa, kwa hiyo njia pekee ya kukabiliana na balaa la nja msimu huuo,ni
kununua chakula mapema”.
Kaimu
Mkuu huyo wa wilaya,alisema kwa hali hiyo,upo umuhimu mkubwa baadhi ya
mifugo ikauzwa mapema,ili michache itakayobaki ipate angalau malisho ya
kutosheleza.
Kwa
upande wake mkulima wa kijiji cha Pohama alikozaliwa waziri wa
maliasili na utalii Lazaro Nyalandu, John Kipandwa,alisema kuwa ukame wa
msimu huu ni mkali mno na kwa vyo vyote wananchi na mifugo yao
wataathirika vibaya, hasa kuanzia miezi ya mwisho mwaka huu na mwanzoni
mwakani.
“Wafugaji
wengi huku kwetu na majirani zetu wameisha baini kuwepo kwa upungufu wa
malisho na maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao, na tayari
wameisha anza hatua ya kuuza baadhi”,alisema Kipandwa.
credit-moblog