Pages

Friday, September 15, 2017

BALOZI WA IRELAND ATEMBELEA MKOANI SINGIDA NA KUAHIDI KUSAIDIA UJENZI WA MABWAWA.

Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock leo amefanya ziara mkoani Singida na kuahidi kuangalia namna ya kufadhili ujenzi wa mabwawa ili yaweze kusaidia kilimo cha umwagiliaji na sio kutegemea mvua pekee.

Mhe. Sherlock amewatembelea wanufaika wa misaada wanayotoa katika Vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi vya Siuyu na Faraja, mara baada ya yeye na mabalozi wengine kumaliza shughuli maalumu bungeni Dodoma.

Ameeleza kuwa amefurahishwa na hali ya hewa ya Mkoa wa Singida huku akisema kuwa uwepo wa barabara nzuri umerahisisha safari yake Mkoani hapa ambapo ni jirani na makao makuu ya nchi.

Mhe. Sherlock ameongeza kuwa anautazama mkoa wa Singida katika sura ya maendeleo zaidi kutokana na fursa zilizopo huku akiahidi kuanzisha miradi itakayosaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la alizeti linalozalishwa kwa wingi Singida. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema ameupokea ujio wa balozi huyo kwa furaha kubwa kwakuwa hiyo ni ishara ya kufunguliwa zaidi kwa milango ya mahusiano mazuri. 

Dkt Nchimbi amesema moja ya faida ya Singida kuwa jirani na makao makuu ni kupata wageni ambao wanaitazama Singida kwa mtazamo wa maendeleo zaidi na ishara Singida itapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

Amesema kilimo cha umwagiliaji kina tija zaidi kuliko kutegemea mvua pekee ambapo Singida inajipanga kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula nchini huku ikiwa na lengo la kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya makao makuu ya nchi ambayo maeneo mengi yatakuwa na shughuli za kiofisi zaidi.

Dkt Nchimbi amesisitiza Mkoa wa Singida hauna njaa, sio masikini na wala sio kame na wananchi wa singida wamejipanga kutumia fursa zozote zinazojitokeza kwa ajili la kukuza uchumi.

Aidha amewataka wananchi wa Singida kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuwa washiriki wakubwa katika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda.

































Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimsisitizia jambo Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock walipokuwa wakiagana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

































Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi akiagana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock, nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 

































Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akifurahia jambo Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock walipokuwa wakiagana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi na wa kwanza kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
































Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.

Thursday, March 26, 2015

Singida watahadharishwa na baa la njaa, washauriwa kutunza vyakula

DSC07291
Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, Edward Ole Lenga, akizungumza kwenye hafla ya utundikaji mizinga ya nyuki kimkoa zilizofanyika katika kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama.Wa pili kulia walioketi ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na (wa kwanza kulia) ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama, James. Kushoto (aliyekaa) ni Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan.
Na Nathaniel Limu, Singida
KAIMU mkuu wa wilaya ya Singida, Edward Ole Lenga, amewataka wakazi wa wilaya hiyo wahakikishe wanahifadhi na kutunza vizuri chakula cha kutosha mwaka mzima,ili kujikinga na balaa la njaa linatishia msimu huu kutokana na mvua chache mno kunyesha.
Lenga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama,ametoa wito huo muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, kuhutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Mgori jimbo la Singida kaskazini  kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kitaifa ya utundikaji wa mizinga ya nyuki ambapo kimkoa yalifayika katika kijiji cha Pohama.
Alisema mvua za msimu huu zimenyesha kwa kipindi kifupi mno na kukatika mapema,kitendo kinachosababisha karibu  mimea yote ikiwemo ya mazao ya chakula  kukauka kabla haijakomaa.
“Siku zote mkuu wetu wa mkoa Dk.Kone amekuwa akiwahimiza wakulima kulima mazao yaliyopewa kipau mbele na mkoa ambayo baadhi ni uwele,mtama na jamii ya Kunde. Mazao haya na mengine yaliyopewa kipaumbele kwa vile yanastahimili hali ya hewa katika mkoa wetu ambao ni ya ukame unaosababishwa na mvua haba. Endapo msimu huu kutakuwa na mkulima aliyelima Mahindi na zao lo lole ambalo halipo kwenye vipaumbele vya mkoa, itakuwa imekula kwake”,alifafanua.
Alisema kwa kifupi,msimu huu sio mzuri kwa upande wa kilimo kutokana na mvua kukatika mapema na hivyo ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha i wananchi wafanye juhudi mapema ya kuhakikisha wanakuwa na chakula cha kukidhi mahitaji.
Aidha,Lenga ametumia fursa hiyo pia kuwahimiza wafugaji wa mifugo kuuza baadhi mapema,ili waweze kununua chakula/nafaka kitakachokidhi mahitaji ya mwaka mzima.
Akifafanua zaidi,alisema “ukame wa mwaka huu, umesababisha pia kuwepo kwa uhaba mkubwa wa malisho ya mifugo na maji pia. Hali hii inaweza kusababisha mifugo kukonda na hivyo baadae itakosakabisa soko zuri au isiuzike kabisa, kwa hiyo njia pekee ya kukabiliana na balaa la nja msimu huuo,ni kununua chakula mapema”.
Kaimu Mkuu huyo wa wilaya,alisema kwa hali hiyo,upo umuhimu mkubwa baadhi ya mifugo ikauzwa mapema,ili michache itakayobaki ipate angalau malisho ya kutosheleza.
Kwa upande wake mkulima wa kijiji cha Pohama alikozaliwa waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu, John Kipandwa,alisema kuwa ukame wa msimu huu ni mkali mno na kwa vyo vyote wananchi na mifugo yao wataathirika vibaya, hasa kuanzia miezi ya mwisho mwaka huu na mwanzoni mwakani.
“Wafugaji wengi huku kwetu na majirani zetu wameisha baini kuwepo kwa upungufu wa malisho na maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao, na tayari wameisha anza hatua ya kuuza baadhi”,alisema Kipandwa.

credit-moblog

Saturday, February 28, 2015

Breaking News: Captain John Komba Afariki Dunia

Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
Eatv imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge ndugu Owen Mwandumbya, Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea simu
source: EATV

Saturday, January 24, 2015

Breaking News: Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu nafasi yake


   Habari kutoka katika mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (pichani) na wanahabari ofisini kwake Dar es salaam muda huu zinasema kiongozi huyo ameamua kubwaga manyanga. Sababu na habari kamili ya hili tutawaletea punde baada ya mkutano huo kwisha.

Ila kasema ameamua kujiuzulu kwa kile alichotaja kuiachia serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo. Stay tuned for more....

source; Michuzi blog

Saturday, June 28, 2014

madereva wa mabasi wayasusa magari yao mkoani Singida jioni hii


  
Madereva wa Mabasi yanayokwenda katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Kagera jioni hii wameingia kwenye mgomo wa kutosafirisha abiria wakiwa mkoani Singida, kwa madai kwamba wanatozwa faini kubwa sana na Askari wa Usalama barabarani mkoani hapo.Baadhi ya abiria wanaosafiri na mabasi hayo wameulalamikia uamuzi wa madereva hao, kwani ni kama wanapewa adabu kwa uamuzi huo.Globu ya jamii inaendelea kufatilia sakata hilo kwa ukaribu zaidi na tutaendelea kufahamishana zaidi.


  


source:Michuzi

Tuesday, May 27, 2014

MO ATAKA MADHEBEBU DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU


Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.


Na Nathaniel Limu, Singida

MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.

Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.

Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.



Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.

"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila vikwazo",amesema.

Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.

"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya dini",amesema.

Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.

source-michuzi blog